DukaDiary ni mfumo wa kimtandao unaokusaidia kurekodi na kuangalia mwenendo wa mauzo, hifadhi taarifa za bidhaa, kurekodi na kufuatilia ulipaji madeni n.k, yote haya kwa kutumia simu au kompyuta yako tu.
Anza Kurekodi MauzoJiunge na mamia ya wafanyabiashara wanaotumia DukaDiary kuendesha biashara zao leo.
Jiunge SasaMfumo upo kwa lugha ya kiswahili, huhitaji kuwa mtaalamu wa kompyuta au mtandao ili uweze kuutumia. Kila kitu kimerahisishwa ili kukuwezesha kufanya shughuli zako za kibiashara kwa uwepesi, bila kuhangaika au kukuchanganya. Iwe unatumia simu au kompyuta kila kitu kitakwenda sawa.
Huhitaji kuwa na daftari wakati wote, mfumo unakusaidia kurekodi mauzo yako, sajili na angalia orodha ya bidhaa zote ulizonaso, tunza taarifa za wateja wako wa mara kwa mara, bila kusahau kutunza kumbukumbu za matumizi na manunuzi yaliyofanyika n.k
Kwa wateja wanaonunua vitu kwa mkopo au kulipa kidogo kidogo, sasa kwa urahisi unaweza kufuatilia madeni yaliyopo na kutunza kumbukumbu za ulipaji madeni. Mfumo utakupigia hesabu ya jumla ya madeni yaliyopo na wateja gani bado hawajalipa ili uweze kuchukua hatua zaidi.
Biashara yako inaendelea kuimarika hata usipokuwepo. Kwa kusajili muuzaji, unaweza kuona mwenendo wa biashara yako popote ulipo na kukusadia kuokoa muda na gharama.
Pata ripoti tofauti zitakazokupa taarifa za biashara yako kwa kina zaidi. Usiumize kichwa kufahamu faida au hasara iliyopatikana, bidhaa zinazotembea au zisizouzika, mwenendo wa mauzo kama yameongezeka au kushuka n.k Mfumo utachakata na kukupa ripoti hizi na nyinginezo bila kuhitajika kupiga mahesabu mwenyewe.
Kwa kifurushi chochote utakachochagua, tumia kwa siku 15 bure kabla ya kulipia.